Siwezi kuzuia machozi yasinitoke, kiuhalisia haikuwa haki kwamba maisha yako duniani yaishie hapa, hakika bado tulikuwa tunakuhitaji baba yetu.
Najua binadamu hatuwezi kufanana kimtazamo, kuna ambao huenda wanasherehekea kutokuwepo kwako leo, lakini mimi, moyo wangu umejeruhika kwa maumivu makali sana.
Ulikuwa na mipango mingi mema juu ya taifa lako, mzalendo uliyejitoa bila uwoga, ulipigana kufa kupona kutetea rasilimali za taifa lako huku ukiwatetea na kuwalinda wanyonge wako.
Baba, taifa litakukumbuka milele. Binafsi nitakuweka wakati wote moyoni mwangu nami nitasimulia vizazi vyangu habari zako njema. Pumzika kwa amani baba, rafiki na kipenzi cha watanzania.
No comments:
Post a Comment